Marekani yadai wadukuzi wa China wameiba TZS bilioni 46 za msaada wa UVIKO-19

0
22

Wadukuzi wanaohusishwa na Serikali ya China wameiba karibu dola milioni 20 [TZS bilioni 46.6] ambazo ni fedha za msaada za Serikali ya Marekani kwa ajili ya Virusi vya Ugonjwa wa Korona (UVIKO19).

Waendesha mashtaka wa Marekani wameishutumu kikundi cha udukuzi APT41 kwa kufanya kazi kwa niaba ya shirika la kijasusi la kiraia la China, na kudai kuwa watendaji wa APT41 walikuwa sehemu ya mipango ya udukuzi ambayo ililenga wanasiasa wanaounga mkono demokrasia huko Hong Kong.

Msemaji wa Idara ya Kijausisi (Secret Service), Justine Whelan amesema wadukuzi hao walivamia fedha za bima ya ukosefu wa ajira na fedha za mkopo za utawala wa biashara ndogo katika zaidi ya majimbo 12 ya Marekani.

Mahakama yasema kuondolewa kwa CAG, Prof. Assad kulikuwa batili

Kampuni ya usalama wa mtandao ya Mandiant, ambayo inamilikiwa na Google, ilisema mwezi Machi kuwa kundi hilo limefanya udukuzi dhidi ya mashirika ya serikali ya Marekani mwaka 2021 na 2022, na kuvunja kompyuta katika mashirika ya serikali takribani majimbo sita ya Marekani.

Hata hivyo, bado haijabainika iwapo wadukuzi hao walifanya wizi huo kwa manufaa yao binafsi au walikuwa wakiendesha shughuli hizo kwa niaba ya Beijing.

Send this to a friend