
Marekani imeitaka Rwanda kuyaondoa majeshi yake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya pande hizo mbili kutia saini makubaliano ya amani.
DRC imekuwa ikiishutumu vikali Rwanda kuunga mkono kundi la waasi la M23, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha mara kwa mara ikisema kuwa inalinda mipaka yake.
Rwanda bado haijatoa msimamo wake kuhusu rasimu hiyo ya makubaliano. Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe ameliambia shirika la Reuters kuwa wataalamu kutoka Congo na nchi yake watakutana wiki hii mjini Washington kujadili zaidi makubaliano hayo.