Marekani yaitaka Rwanda kusitisha mapigano DRC

0
5

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeishinikiza Rwanda kusitisha mapigano mara moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku ikitoa tahadhari juu ya kuunga mkono kundi la M23 lililoteka mji wa Goma.

Katika mazungumzo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Waziri Marco  Rubio amesisitiza kuwa Marekani inasikitishwa sana na kuongezeka kwa mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC.

Hata hivyo, Rwanda imekanusha mashtaka ya kutaka kudhibiti madini DRC, ikisema lengo lake ni kukabiliana na kundi lenye silaha liitwalo FDLR, ambalo linaundwa na wanamgambo wa Kihutu kufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Hivi karibuni, M23 wamevamia mji wa Goma na kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege. Hata hivyo, Marekani kwa miaka mingi imeionya Rwanda kuhusu uungaji mkono wake kwa M23.