Marekani yamuua kiongozi wa kundi la Dola ya Kiislam (IS)

0
41

Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza taarifa ya  kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Dola ya Kiisalamu (Islamic State-IS) nchini Syria, Abu Ibrahim al- Hashimi al- Quraysh, wakati wa shambulio lililofanywa na wanajeshi maalum wa Marekani nchini humo leo.

Taarifa kutoka White House zinasema kuwa, kiongozi huyo wa IS alijilipua yeye pamoja na familia yake ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi. Biden ameongeza kuwa kiongozi huyo alihusika kwenye mashambulio pamoja na mauaji ya watu wengi huko Iraq.

Abu Ibrahim al- Hashim alizaliwa mwaka wa 1976 katika mji wa Mahlabiya, Kaunti ya Ninenah. Alikuwa na wake wawili na watoto 7. Baba yake alikuwa Imamu katika msikiti wa Furgan huko Mosul kuanzia mwaka 1982-2001

Al-Qurayshi alikuwa na wadhfa wa Naibu wa IS ambaye alimrithi Abu Bakr al-Baghdadi alipofariki kama mkuu wa kundi hilo.

Inaaminika alijiunga na na kundi hilo mwaka 2003/04, akiwa ni mtu anayeelezwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kijeshi na kijasus, pia alikuwa mhusika mkuu katika operesheni za IS.

Marekani ilikuwa imeahidi zawadi ya dola milioni 10 kwa mtu yeyote ambaye angesaidia kupatikana kwa kiongozi huyo.

Send this to a friend