Marekani yamuwekea vikwazo mfanyabiashara wa Zimbabwe

0
49

Marekani imemuwekea vikwazo mfanyabiashara mkubwa wa Zimbabwe kwa tuhuma kujihusisha na rushwa na kutoa msaada kwa maafisa wa juu wa serikali.

Wizara ya Fedha imesema kuwa itashikilia mali zote za Kudakwane Tagiwirei zilizopo Marekani pamoja na kampuni yake ya Sakunda Holdings.

Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kufanya biashara isiyo wazi ambayo imekuwa ikimuingizi mamilioni ya dola.

Wizara hiyo imesema mfanyabiashara huyo amekuwa akitumia uhusiano wake na maafisa wa serikali ya Zimbabwe, akiwemo Rais, kujipatia zabuni za kitaifa.

Anapopewa zabuni hizo, yeye huwapa washirika wake magari ya kifahari.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo hajasema lolote juu ya tuhuma hizo.

Send this to a friend