Marekani yamwekea vikwazo Spika wa Bunge la Uganda na mumewe

0
46

Marekani imewawekea vikwazo maafisa watano wa Uganda, akiwemo Spika wa Bunge la nchi hiyo, Anita Among, mumewe na Naibu Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Ulinzi kutoingia nchini humo kwa tuhuma za ufisadi na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imesema kuwa Spika Among amewekewa vikwazo kutokana na kuhusika kwake katika ufisadi mkubwa unaohusishwa na uongozi wake wa kibunge, huku Naibu mkuu wa zamani wa jeshi la Uganda, Luteni Jenerali Peter Elwelu akiwekewa vikwazo kutokana na ‘mauaji ya kiholela’ yaliyofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo.

Marufuku ya kuingia nchini humo inakuja mwezi mmoja tu baada ya Uingereza pia kutangaza vikwazo sawa na hivyo dhidi ya Spika na mawaziri wawili wa zamani ambayo imesababisha kufungiwa kwa mali yake na fedha huko London.

Ripoti yabaini dhahabu ya mabilioni ya dola husafirishwa kimagendo kutoka Afrika

Vikwazo hivyo vya Uingereza vimesababisha uchunguzi, huku mashirika na maafisa wengi wa serikali, akiwemo Rais Yoweri Museveni akimtaka Spika kueleza madai hayo ya mali na fedha nchini Uingereza.

Kwa upande wake Waziri wa habari wa nchini humo, Dkt. Chris Baryomunsi amesema anashangazwa kwa viongozi hao kuwekewa vikwazo wakihusishwa na kesi ya ufisadi ambayo bado haijafanyiwa maamuzi na mahakama.

Send this to a friend