Marekani yatishia kupiga marufuku mtandao wa TikTok

0
47

Serikali ya Marekani imewataka wamiliki wa TikTok kutoka nchini China kuacha hisa zao katika programu hiyo maarufu ya video au vinginevyo watapigwa marufuku na nchi hiyo.

Programu hiyo ya video inayomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance inashutumiwa kuwa hatari kwa usalama wa taifa kupitia data zilizokusanywa kutoka kwa mamilioni ya watumiaji.

Kwa miaka mingi, maafisa na wabunge wa Marekani wameibua wasiwasi kwamba data za watumiaji wa programu hiyo maarufu zinaweza kuangukia mikononi mwa serikali ya China.

Jinsi ya kuondoa taarifa zako binafsi Google

Hii ni mara ya kwanza chini ya utawala wa Rais Joe Biden kutoa onyo hilo la kupiga marufuku baada ya Rais Mstaafu, Donald Trump wa Republican kujaribu kupiga marufuku mtandao wa TikTok mnamo 2020 lakini alizuiwa na mahakama za Amerika.

ByteDance ilithibitisha kuwa asilimia 60 ya hisa zake zinamilikiwa na wawekezaji wa kimataifa, asilimia 20 na wafanyakazi huku asilimia 20 zikimilikiwa na waanzilishi wake.

 

Send this to a friend