Marekani yavunja uhusiano na Shirika la Afya Duniani

0
46

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuuvunja uhusiano kati ya nchi hiyo na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hatua hiyo inatajwa kuwa ni muondelezo wa Marekani kuoneshwa kutorishishwa kwake na utendaji wa shirika hilo ambalo mara kadhaa imekuwa ikilituhumu kutotekeleza majukumu yake kutokana na kutoiwajibisha China kufuatia mlipuko wa virusi vya corona.

“China inalimiki Shirika la Afya Duniani (WHO),” amesema Rais Trump wakati akitoa maazimia hayo.

Marekani imesema kuwa itatumia fedha ilizokuwa inaipa WHO kuwenye mashirika mengine.

WHO haijasema lolote kuhusu uamuzi huo, lakini Umoja wa Ulaya (UE) umeitaka nchi hiyo kufikiri upya juu ya uamuzi huo kwa maelezo kuwa utakwamisha jitihada za kupambana dhidi ya janga la corona.

Mwezi uliopita Rais Trump alitangaza kuwa angesitisha kulifadhili shirika hilo endapo lisipofanya mabadiliko makubwa ndani ya siku 30.

Send this to a friend