Marekani yazuia Chuo cha Harvard kudahili wanafunzi wa kigeni

0
4

Serikali ya Marekani imekifungia Chuo Kikuu cha Harvard kudahili wanafunzi wa kimataifa, na kuamuru wanafunzi wa kigeni waliopo wahamie vyuo vingine au wapoteze sifa ya kisheria ya kuishi nchini humo.

Uamuzi huo umetokana na madai kuwa chuo hicho kinachochea vurugu na chuki dhidi ya Wayahudi, na kushirikiana na Chama cha Kikomunisti cha China ndani ya chuo.

Katika taarifa yake, Chuo Kikuu cha Harvard kimelaani hatua hiyo kikiiita kinyume cha sheria na kitendo cha kulipiza kisasi.

“Tumejitolea kikamilifu kudumisha uwezo wa Harvard wa kukaribisha wanafunzi na wasomi wetu wa kimataifa, ambao wanatoka zaidi ya nchi 140 na ambao wanakiimarisha chuo hiki na taifa hili  kwa kiwango kisichoelezeka,” chuo hicho kimesema.

Send this to a friend