Marioo adaiwa milioni 550 kwa kuvunja mkataba

0
54

Msanii wa muziki, Omary Mwanga maarufu ‘Marioo’ anayedaiwa TZS milioni 550 kwa madai ya kuvunja mkataba, anatarajiwa kufika mahakama Kuu Masjala ya Wilaya ya Arusha Machi 18 na 19 mwaka huu kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo.

Marioo pamoja na meneja wake, Sweetbert Mwinula wanadaiwa kuvunja mkataba wa kutumbuiza katika hafla ya Mr & Miss Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini madai yaliyotolewa na kampuni ya Kismaty inayojihusisha na kuandaa matukio ya burudani mbalimbali nchini.

Kampuni hiyo imedai kwamba Septemba 23, 2021 iliingia mkataba na Marioo kutumbuiza katika shindano hilo kwa gharama ya TZS milioni 15 katika tukio lililopagwa kufanyika Septemba 24 na hafla nyingine iliyopangwa kufanyika Septemba 25 Blue Stone Lounge huku ikieleza kuwa Septemba 17 iliwalipa wadaiwa TZS milioni 8 na wakati wa kutia saini iliwalipa TZS milioni 15.

Zuchu apigwa marufuku kufanya muziki Zanzibar kwa miezi sita

Kampuni hiyo imedai kuwa Septemba 25 wadaiwa hawakuonekana kwa ajili ya kutumbuiza Blue Stone kama ambavyo walikubaliana katika mkataba.

Mdai ameeleza kuwa kutokana na kutoonekana siku hiyo iliingia hasara ya TZS milioni 500 na hasara nyingine ya TZS milioni 50 ambayo ilitokana na kukaribisha wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa hoteli kubwa, fedha walizolipwa na pia kupoteza biashara na kukosa kipato.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend