Marubani waliogoma Kenya wapewa saa 24 kurejea kazini

0
40

Takribani abiria 10,000 wameathiriwa kufuatia mgomo wa marubani wa Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways (KQ) ulioanza leo Novemba 5, 2022 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.

Chama cha Marubani wa Mashirika ya Ndege ya Kenya (KALPA) kimesema hakuna ndege ya Shirika hilo takribani 15 iliyosafirishwa na wanachama wake ambayo imeondoka kwenye Uwanja huo kuanzia saa 12:00 asubuhi.

Mufti awashauri Watanzania kuacha dhambi ili mvua zinyeshe

“Mgomo unatekelezwa kikamilifu,” amesema Katibu Mkuu wa KALPA, Murithi Nyagah katika taarifa iliyotolewa mapema leo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Kenya, Allan Kilavuka, ametoa saa 24 kwa marubani waliogoma kurejea kazini na kwamba vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

KQ imesema itapoteza Ksh milioni 300 (TZS Bilioni 5.7) kwa kila siku ya mgomo, huku tani 600 za mizigo zikikwama.

Marubani hao takribani 400 walitangaza mgomo baada ya kuilalamikia Kenya Airways kushindwa kulipa madai yao ya michango ya pensheni na malipo yaliyoahirishwa baada ya notisi ya siku 14.

Send this to a friend