Marufuku kurusha matangazo ya tiba asili bila kibali

0
65

Baraza la Tiba Asili na na Tiba Mbadala limepiga marufuku matangazo yote ya tiba asili na tiba mbadala katika vituo vya habari na mitandao ya kijamii na kuzuia uuzaji holela wa dawa, ikiwemo kwenye vyombo vya usafiri, nyumba za ibada na masoko.

Mwenyekiti wa Baraza, Prof. Hamis Malebo amesema matangazo yote ni lazima yapate kibali cha baraza kabla ya kurushwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Matangazo yote ambayo hayakupitishwa na baraza yamesitishwa kuanzia leo [jana]. Kwa pamoja tuhakikishe huduma zote zinatolewa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo,” ameelekeza,

Aidha, amewataka waganga wote wanaotoa tiba bila usajili kukamilisha usajili wao kabl ya Machi 31 mwakani, baada ya hapo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ameelekeza dawa zoe kuuzwa katika maduka ya tiba asili yaliyosajiliwa.

Hadi Novemba 30, 2021 waganga 29,459 , vituo 1,077 na dawa 67 vilikuwa vimesajiliwa na baraza hilo, usajili ambao ulianza mwaka 2010.

 

Send this to a friend