Marufuku ulaji nyama ya nguruwe

0
114

Wakazi wa Kata ya Tandala wilayani Makete, mkoani Njombe wamepigwa marufuku kuchinja na kula nyama ya nguruwe kwa muda usiojulikana kutokana na uwepo wa ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Akitoa agizo hilo, Ofisa Mifugo na Uvuvi wilayani humo, Aldo Mwapinga amesema katika Kata hiyo kumeripotiwa dalili za ugonjwa huo na tayari kuna vifo 21 vya nguruwe.

Mchungaji jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

“Baada ya kupata taarifa hizi tumesimamisha zoezi la uchinjaji wa nguruwe katika kila eneo la Kata ya Tandala, na pili kutoa nguruwe kuwapeleka kwenye maeneo mengine, pia tumezuia utoaji nguruwe kutoa zizi moja kwenda jengine kwaajili ya kuwapandisha kwa jike,” amesema Mwapinga.

Aidha, amewaomba wananchi kutoa ushirikiano pamoja na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na wataalamu wa mifugo ikiwemo kuacha kufukua nguruwe waliofukiwa baada ya kufa, kuwachinja nakwenda kuuza nyama vilabuni nyakati za usiku.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend