Masauni awataka Trafiki kukamata mabasi yasiyo na vizibiti mwendo

0
49

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini na Baraza la Taifa na Usalama barabarani kuhakikisha wanayakamata mabasi yote yasiyo na vizibiti mwendo

Masauni amesema hayo leo 24 October 2022 wakati akizindua baraza la Taifa la Usalama Barabarani makao makuu ya Nchi Dodoma ambapo, amesema miongoni mwa vyanzo vya ajali Nchini ni mwendo kasi unaosababishwa na madereva wazembe wasio fuata sheria za usalama barabarani kitendo kinachopelekea ajali nyingi hapa Nchini

Pia Maasauni ameliagiza Jeshi la Polisi kuanzia leo 24 October kukamata mabasi yote yasiyo na vizibiti mwendo ambapo amesema kuwa tayari alishatoa maelekezo hayo kuwa ifikapo September mwka huu mabasi yote yawe na vizibiti mwendo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jamanne Sagini ambaye Pia ni Mwenyekiti wa Balaza la Taifa la Usalama barabarani amesema baraza la Taifa la Usalama barabarani kwa kushirikiana na baraza la kazi litaendelea kutoa mafunzo ya Usalama barabarani kwa viongozi wa umma wakiwemo makatibu wakuu na wabunge ili kuwajengea uwezo wa kukemea matukio amabayo yanapelekea ajali kutokea.

Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambaye ni kaimu Mwenyekiti wa baraza hilo, amemshukuru Waziri Masauni kwa kumteua kuwa katika baraza hilo ambapo ameahidi kwakushirikiana na baraza na wadau wa Usalama barabarani na kutatua changamoto zilizopo

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Wilbroad Mutafugwa amesema kuwa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani toka limeanzishwa kusimamia kamati za Mikoa na Wilaya umesaidia ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya fedha zilizotokana na ada za ukaguzi wa magari mbalimbali.

Send this to a friend