Mashabiki wa Arsenal wakamatwa wakisherekea kuifunga Manchester United

0
42

Polisi mjini Jinja nchini Uganda wamewashikilia takribani wafuasi 20 wa klabu ya Arsenal waliokuwa wakisherehekea ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Manchester United katika mitaa ya jiji hilo Jumapili Januari 22 mwaka huu.

Wakati Polisi wakiwa hawajazungumzia tukio hilo, Baker Kasule mmoja kati ya mashabiki waliokuwa katika kundi hilo amedai gari la polisi wa doria lilisimama mbele yao na kuwataka kila mmoja kushuka katika msafara wao uliokuwa na magari matano na kupanda gari la doria lililokuwa likielekea Jinja, Kituo cha Polisi.

Chama cha Soka England chasema goli la Fernandes ni halali

“Sijui tumefanya nini lakini tulikuwa tukisherehekea ushindi wetu dhidi ya wapinzani wetu Manchester United,” amedai Kasule.

Naye Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Polisi cha Jinja, Maurice Niyonzima amekataa kuzungumzia suala hilo, akisema jeshi hilo lina msemaji.

Send this to a friend