Mashabiki wa Yanga wazuia Mayele kuuzwa

0
59

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Young African (YANGA), Senzo Mazingisa amesema kwa sasa viongozi wa klabu hiyo hawana mpango wa kumuuza mchezaji Fiston Kalala Mayele kwa sababu ni kivutio kikubwa cha timu hiyo.

Senzo amesema licha ya kupokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali zikiwemo RS Berkane ya Morocco na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa ajili ya kumsaini nyota huyo, wamekiri kuwa hawawezi kuumuza.

“Tunaweza kutaka kuumza ili tupata hela nyingi, lakini tunawaambia nini mashabiki wa Yanga, Mayele kwa sasa ni lulu katika timu yetu, unapomuondoa uwe na majibu ya kujibu,” amesema.

Aidha, amesema anaamini kuondoka kwa Mayele ni jambo ambalo halitamfurahisha hata kocha wa timu hiyo Nasreddine Nadi kutokana na uwezo wake mkubwa katika klabu ya Yanga.

Senzo amejinadi kuwa, Yanga imejipanga kufanya usajili mzuri kuelekea msimu ujao kwa kufuata ushauri wa kocha Nadi.

Mayele kabla ya kusainiwa na klabu ya Yanga alikuwa akiicheze AS Vita ya DRC nchini Congo, na Tanzania ni nchi yake ya kwanza kucheza soko la kulipwa.

Send this to a friend