Mashabiki wanne wa Namungo wafariki wakiifuata Yanga

0
46

Mashabiki wanne wa Namungo FC wamefariki kwenye ajali eneo la Miteja karibu na Somanga wilayani Kilwa mkoani Lindi wakati wakisafiri kutoka Ruangwa kuelekea mkoani Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga SC.

Katika taarifa iliyotolewa na Namungo imesema imepokea kwa masikitiko ajali hiyo ambayo imejeruhi watu wengine 16 ambao wamepelekwa katika kituo cha afya Tingi wilayani humo kwa ajili ya matibabu.

“Namungo FC tunatoa pole kwa wana-Ruangwa, mashabiki, familia na kwa wote waliopata ajali hiyo na majeruhi tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka,” imesema Namungo.

Namungo imepangwa kukutana na Yanga SC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam leo Septemba 20, 2023 saa moja jioni.

Send this to a friend