Masharti manne yaliopunguzwa Bima ya Afya kwa Wote

0
43

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali imesikia maoni ya Watanzania hivyo kufanya marekebisho ya Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote kwa punguza masharti yatakayomlazimisha mtu kuwa mwanachama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri Ummy ameeleza kuwa muswada wa awali ulifungamanisha huduma muhimu za kijamii tisa ambazo mtu anapokwenda kuziomba lazima awe amejiunga na bima ya afya lakini baada ya kusikiliza maombi ya wadau nne zimeondolewa na kubakia matano.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy Mwalimu huduma zinazopendekezwa kuondolewa ni utambulisho wa namba ya mlipakodi (TIN), usajili wa laini za simu, hati za kusafiri, usajili wa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na utoaji wa kitambulisho cha taifa.

Zitakazobakia ni leseni ya udereva, bima za vyombo vya moto leseni za biashara, visa kwa wageni na usajili wa wanafunzi wa vyuoni.

Jela miaka 30 kwa kumbaka mdogo wake ili awe tajiri

“Dhana ya ufungamanaji inalenga kuwezesha utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, kuweka ulazima wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya na kuweka msukumo wa kila mwananchi kujiunga na bima ya afya kabla ya kuugua,” amesema.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend