Masharti ya Benki Kuu Tanzania kwa wanaofanya biashara ya fedha za kigeni

0
45

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emanuel Tutuba amepiga marufuku taasisi zinazofanya biashara ya fedha za kigeni na madalali wa kimataifa wa fedha hizo ambao hawajasajiliwa ndani ya nchi.

Katika taarifa ya BOT kwa vyombo vya habari, imesema madalali/wafanyabiashara wa fedha za kigeni nchini wanapaswa wakati wote kuzingatia utaratibu wa kumtambua mteja kabla ya kufanya naye biashara hiyo.

Katika maelekezo hayo, kiwango cha juu cha mizania kati ya mali na amana katika fedha za kigeni (foreign exchange Net Open Position (NOP) kitakuwa asilimia 10 ya mtaji wa msingi (core capital) na kinatakiwa kuzingatiwa wakati wake.

Bandari ya Dar es Salaam yaipita Mombasa kwa ufanisi

Aidha, ameelekeza kuwa Barua za Udhamini (Letters of Credit (LCs) za shehena zinazopitia hapa nchini (transit cargoes) zitatokana na fedha za kigeni kutoka katika nchi ambako shehena hizo zinakwenda.

“Inasisitizwa kwamba uzingatiaji wa matakwa yaliyoainishwa hapa ni wa lazima na kutakuwa na usimamizi na ukaguzi kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Kukiuka maelezo haya kutasababisha adhabu kama zinavyoelezwa katika Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992,” ameeleza Tutuba.

Hata hivyo, BOT imeelekeza taasisi za fedha za kigeni kuwa miamala yote ya fedha za kigeni inayozidi thamani ya dola za Kimarekani milioni 1 kwa muamala mmoja katika soko la rejareja, ifanyike kwa bei ya soko la fedha za kigeni baina ya benki huku miamala yote ya mteja mmoja kwa siku kujumuishwa ili kujua jumla ya kiasi husika.

Send this to a friend