Masharti ya NECTA kwa wanaosajiliwa kurudia shule baada ya kujifungua

0
18

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetoa utaratibu la kuwasajili wanafunzi waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito kwa ajili ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Utaratibu huo umetolewa kupitia kwa barua maalum kwa Makatibu Tawala ambayo imeeleza wanaoruhusiwa kufanya mtihani huo ni waliokatisha masomo kwa kupata ujauzito, waliofeli, walioshindwa kufanya mitihani, waliofutiwa matokeo.

Waraka wa Elimu: Vigezo vya kuzingatiwa kurejeshwaji shuleni wanafunzi waliokatiza masomo kwa ujauzito

Utaratibu wa NECTA unahusisha sifa za mwanafunzi ambaye alifanya mtihani na kufaulu mtihani wa upimaji wa darasa la nne na awe amehudhuria elimu ya msingi kwa miaka saba.

Pia, awe alishajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kufeli, kufutiwa matokeo au kushindwa kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali.

Akaunti ya mwanafunzi yafungwa ikiwa na TZS bilioni 2.3

NECTA imeeleza pia kuwa mwanafunzi ataruhusiwa kurudia mtihani mara moja katika mwaka unaofuatia baada ya kushindwa kufanya mtihani wa awali kutokana changamoto alizopata.

Aidha, mtahiniwa anatakiwa kusajiliwa katika shule ya msingi aliyosoma au nyingine atakayoona inafaa ambapo watasajiliwa katika sehemu maalum ya watahaniwa wanaorudia mtihani kwenye mfumo wa usajili wa wanafunzi wa shule za msingi (PRem).

 

Send this to a friend