Masharti ya polisi kwa vijana waliochaguliwa kujiunga Jeshi la Polisi

0
111

Jeshi la Polisi limewataka vijana wote waliochaguliwa kujiunga na jeshi hilo kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia Oktoba 23 mwaka huu wakiwa na TZS 40,000 kwa ajili ya kupima afya.

Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa kwa waliofanyiwa usaili Baracks Dar es Salaam kwenye vikosi ambavyo vipo chini ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi watatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Dodoma 24/10/2021 saa 2.00 asubuhi wakiwa na nauli zao kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.

Orodha ya majina ya vijana waliopata ajira Jeshi la Polisi

Jeshi limeonya kuwa atakayewasili shuleni hapo baada ya Oktoba 29 mwaka huu hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo. Pia, ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakaepatikana na simu atafukuzwa mafunzo mara moja.

Tangazo la nafasi za kazi TAMISEMI

Hivi karibuni jeshi hilo lilitoa orodha ya majina ya vijana 3275 waliochaguliwa baada ya usaili.

Send this to a friend