Mashine ya kunyanyua vitu vizito ya TPA yazama baharini

0
82

Mashine ya kunyanyua vitu vizito (Crane) ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) iliyokuwa ikishushwa kutoka kwenye Meli ya LCT AJE 1 jana Mei 23, 2021 katika Bandari ya Dar es Salaam ilipata ajali ya kutumbukia baharini.

Mashine hiyo yenye uzito wa takribani tani 70, iliwasili kwa meliu kutoka Visiwa vya Songongo na ilikuwa ikishushwa katika eneo la Gati ya Malindi.

TPA imeeleza kuwa ajali hiyo halikusababisha athari yoyote kwa mtu/watu na kwamba zoezi la kuipoa linaendelea.

Send this to a friend