Mashirika 19 ya umma yaunganishwa na kubakia 7

0
50

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema mchakato wa kuyafumua mashirika 19 ya umma umeanza na tayari uamuzi umefanyika wa kuyaunganisha mashirika hayo na kubakiza mashirika saba pekee.

Uamuzi huo ni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza kufanyike mageuzi katika mashirika na taasisi hizo kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi na kuchangia kukuza uchumi wa taifa.

Mchechu amebainisha kuwa “kuna ambayo tayari tumeshaamua kuyaunganisha, ni mashirika 19 yataunganishwa na kubakia saba” amesema huku akieleza kuwa uamuzi huo ni kutokana na mashirika hayo ambayo hakuyataja jina kuwa na shughuli zinazofanana au kushabihiana.

Mahakama yamtambua Doreen kama mnufaika wa mali za Mrema

Aidha, amesema hatua zinaendelea ili kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha mashirika hayo yaweze kutangazwa.

Send this to a friend