Mashirika, taasisi zatakiwa kujikita kuwekeza nje ya nchi

0
36

Taasisi na Mashirika ya Umma nchini yametakiwa kujikita katika kufikiria njia mbalimbali zitakazowawezesha kuwekeza nje ya nchi ili kusaidia nchi iendelee kujitawala kiuchumi.

Ameyasema hayo Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea ufunguzi wa kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kitakachofunguliwa na Rais Samia Suluhu Agosti 28, 2024 katika Kituo cha Mikutano, jijini Arusha.

Mchechu amesema kuwa ili taasisi na mashirika ya umma yaweze kufanikiwa kuwekeza nje ya nchi, lazima kwanza yawe imara ndani ya nchi kwani haiwezekani kuwekeza nje ya nchi kama ndani ya nchi taasisi haiko imara.

Ameongeza kuwa, utendaji kazi wa taasisi za umma unatakiwa kubadilika ili kuwa na mawazo mapana yatakayowawezesha kuwekeza nje ya nchi na kwamba taasisi zina wajibu wa kuwa na mipango ya muda mrefu ili ziweze kuchangia kwenye mpango mkakati wa nchi wa mwaka 2025 na sio kusubiri Tume ya Mipango ifanye yenyewe.

Send this to a friend