Mastaa wa Bongo wanaotarajia kufunga ndoa 2022

0
33

 

Kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, mwaka 2021 ulikuwa wa kutoa album na EPs, lakini huenda mwaka 2022 ukawa ni wa kufunga pingu za maisha kwa mastaa wengi.

Wanaotarajiwa kufunga ndoa mwaka huu ni wale ambao tayari wamevisha au kuvishwa pete za uchumba. Hata hivyo yawezekana wakawepo watakaovishana mwaka huu na kuoana. Ndoa zinazotaraijiwa ni kutoka kwa;

1. Vanessa Mdee
Alivishwa pete ya uchumba Desemba 2020 na mchumba wake Rotimi ambaye ni mwigizaji na mwanamuziki kutoka Marekani mwenye asili ya Nigeria. Wawili hawa walijaliwa mtoto Sepremba 2021.

2. Nandy na Bil Nas
Aprili 2020 alivishwa pete ya uchumba na Bilnas, na amekuwa akieleza kwamba anaitamani ndoa. Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba Nandy ni mama kijacho.

3. Queen Poshy
Mrembo huyo alivishwa pete ya uchumba Julai 2020 na tayari wamejaliwa mtoto. Poshy amesema kwamba mchumba wake anaishi Dubai na ndio sababu hawaonekani pamoja mara nyingi.

4. Jacqueline Wolper na Rich Mitindo
Wawili hawa wana mtoto na Agosti 2021 Wolper alivishwa pete ya uchumba. Licha na matarajio ya ndoa, wamekuwa na milima na mabonde kwenye uhusiano wao ambapo kuna kipindi waliachana na kila mmoja kwenda njia yake.

5. Rosa Ree
Septemba 2021 alivishwa pete na mchumba wake King Petrouse, ambaye si mtu anayefahmikia sana. Inadaiwa kwamba wawili hao walifahamiana tangu wakisoma sekondari.

6. Dogo Janja
Ngarenaro Republic huenda mwaka huu ikajawa na vifijo pale Janjaro atakapokula kiapo cha maisha mbele ya mchumba wake Queen Linah. Tayari mrembo huyo amevishwa pete Aprili 2020. Janjaro amewahi kuwa na uhusiano na Irene Uwoya, uhusiano ambao ulivunjia baadaye.

7. Darassa
Agosti 2021 aliona yaishe akapiga goti na kumvisha pete ya uchumba kwa mzazi mwenzake.

8. Stamina
Kabwela kutoka Morogoro alipiga hatua nyingine kwenye uhusiano wake alipoamua kumvisha pete mchumba wake Agosti 2021. Huko nyuma amewahi kuoa, lakini ndoa hiyo ilivunjika baada ya muda mfupi.

Je! unadhani staa gani mwingine huenda akafunga ndoa mwaka huu?

Send this to a friend