Maswali 7 ya kujiuliza kabla ya kuacha kazi yako

0
94

Watu wengi huacha kazi kutokana na misukosuko midogo na kujikuta wakiingia kwenye matatizo makubwa.

Kabla hujaamua kuiacha kazi yako, hakikisha kwanza unafikiria mambo haya yafuatayo ambayo yatakusaidia kukupa uhakika wa maamuzi yako.

Sababu
Sababu yako ni ya msingi? Hakikisha unakuwa na sababu sahihi inayokufanya uache kazi. Usichukue uamuzi wa kuiacha kazi yako kwa mambo madogo ambayo ungeweza kuyavumilia.

Muda
Kufanya jambo lolote nje ya wakati ni kosa kubwa. Hakikisha uamuzi unaoufanya kwa wakati huo unaufanya kwa wakati sahihi.

Kipato
Inawezekana kazi unayotaka kuiacha ndiyo chanzo chako pekee cha kipato, hivyo ni vyema utafute chanzo kingine cha kipato kwanza.

Kazi nyingine
Usiache kazi kabla ya kufahamu kama utapata kazi sehemu nyingine, kwani kuacha kazi bila kulifahamu hili kutakuweka katika hali ngumu ya kuanza upya.

Shirikisha watu wa karibu
Ni vyema ushirikishe watu wa karibu yako ikiwa ni pamoja na familia, kwani pasipokufanya hivyo kunaweza kukuweka katika mgogoro na familia yako.

Weka Akiba
Akiba ni muhimu kwa ajili ya kukusaidia wakati ambao hauna kipato cha kutimiza mahitaji yako. Hakikisha unabainisha matumizi yako ya kifedha na kuhakikisha una akiba.

Kurudi kwa mwajiri wako
Je! Kabla ya kuacha kazi yako unafahamu kama unaweza kuruhusiwa kurudi kazini ikiwa mambo yatakwenda vibaya? Jambo hili ni a msingi pia.

Ukizingatia mambo haya yote, sasa unaweza kufanya uamuzi ulio sahihi.

Send this to a friend