Mataifa 10 ya Afrika yanayotarajia kupokea msaada mkubwa kutoka Marekani 2025

0
26

Katika hatua ya kushangaza, mataifa mengi yanayopokea msaada wa kigeni, Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza kusitisha ufadhili wa USAID kwa nchi kadhaa, uamuzi ambao umetikisa sekta muhimu kama afya, kilimo, na elimu katika mataifa yanayoendelea.

Licha ya kusitishwa kwa miradi ya USAID, data kutoka kwenye tovuti ya Misaada ya Kigeni ya Marekani (US Foreign Assistance website), inaonesha kuwa Marekani bado imejitolea kusaidia mataifa mengi ya Afrika kupitia fedha zilizotengwa. Idara zingine kama Wizara ya Kilimo na Tume ya Biashara ya Shirikisho zinaendelea kutoa ufadhili kwa nchi zinazoendelea.

Pamoja na kusitisha miradi ya USAID, Marekani bado imeahidi msaada mkubwa wa kifedha kwa mataifa mbalimbali ya Afrika.

Nchi 10 za Afrika zenye furaha zaidi mwaka 2025

Hapa ni orodha ya nchi 10 za Afrika ambazo zimepewa ahadi ya kupokea msaada mkubwa kutoka Marekani mwaka 2025, licha ya kusitishwa kwa ufadhili wa USAID (TZS);

1. Sudan: Bilioni 660.2
2. Ethiopia: Bilioni 493.5
3. Somalia: Bilioni 373.3
4. Kenya: Bilioni 341.3
5. Tanzania: Bilioni 275
6. Rwanda: Bilioni 264.8
7. Afrika Kusini: Bilioni 239.58
8. Msumbiji: Bilioni 213.9
9. Misri: Bilioni 204.3
10. Uganda: Bilioni 160.3

Chanzo: US Foreign Assistance website