Utafiti mpya uliotolewa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kupambana na Matumizi Mabaya ya Pombe na Madawa ya Kulevya nchini Kenya (NACADA) unaonyesha kuongezeka kwa matumizi ya mihadarati nchini humo na kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu kuenea kwa matumizi ya bangi miongoni mwa vijana wadogo.
Kwa mujibu wa ripoti ya NACADA, idadi ya watu wanaotumia bangi nchini humo imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka 5.
Takwimu zinaonyesha kuwa umri wa chini wa kuanza kutumia vilevi mbali mbali ikiwa ni pamoja na tumbaku, pombe, na madawa ya kulevya ni mdogo sana, hadi watoto wenye umri wa miaka sita wameingizwa katika matumizi ya tumbaku.
Imeonekana pia matumizi ya madawa ya kulevya kama vile heroni, huanza kutumiwa miongoni mwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka minane na kumi na minne, wakati matumizi ya kokeini huanza katika umri wa miaka ishirini.
Chanzo: BBC Swahili