Dawa za kulainisha choo zinavyochangia mawe kujaa kwenye figo

0
60

Matumizi holela ya dawa za kulainisha choo ‘laxactive’ yamedaiwa kuwa moja ya chanzo cha kuathiri mfumo wa chakula pale zinapotumika bila maelekezo ya daktari.

Akitolea ufafanuzi, Muuguzi Msaidizi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Paschael John amesema dawa hizo zinapotumika kiholela hulazimisha maji kukusanyika katika matumbo kwa dharura kutoka kila pembe ya mwili ili kusaidia kulainisha choo, hatimaye humfanya mgonjwa apate kuhara ambako huchangia kuharibika kwa mfumo wa chakula.

Watoto 18 wafariki baada ya kunywa dawa yenye ‘sumu’

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure, Bahati Msaki amefafanua kuwa dharura ya kukusanyika kwa maji katika tumbo husababisha sehemu nyingine za mwili ikiwemo figo kupungukiwa maji, hivyo kusababisha kuwepo na tatizo la mawe kwenye figo.

Ameongeza kuwa maji yanapopungua kwenye mfumo wa utoaji taka mwili nje, hupelekea mkojo kubadilika rangi na kuwa wa njano pamoja na kutoa harufu kali, hivyo kwa wenye tatizo la kupata choo kigumu ni vyema kuwasiliana na wataalamu ili kufuata njia za asili za kutatua changamoto hiyo bila kutumia dawa.