Mauaji watu saba Kigoma chanzo ni wivu wa mapenzi, mtuhumiwa akamatwa
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Peter Mors, mkazi wa Mlole Kata ya Mwanga Kaskazini, kwa tuhuma za mauaji ya watu saba wa familia moja.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Peshi la Polisi, CP Liberatus Sabas amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, na kueleza kuwa jeshi limejiridhisha kuwa Mors amefanya mauaji hayo kwa sababu ya wivu wa mapenzi .
Watu saba wa familia moja waliuawa kwa kukatwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Kiganza, mkoani Kigoma.