Mauaji ya Daktari Tarime: Wananchi walalamikia Jeshi la Polisi

0
47

Wakazi wa Kata ya Nyamongo, Tarime Vijijini mkoani Mara wameilalamikia Jeshi Polisi juu ya kutokuwepo kwa taarifa rasmi wala watu waliokamatwa hadi sasa kufuatia tukio la mauaji ya Mganga Mfawithi wa kituo cha afya cha Nyangoto, daktari Isack Sima.

Wananchi wamelaani tukio hilo lililotokea Mei 03, 2023 baada ya daktari huyo kuvamiwa na watu wasiojulikana na kuuawa kwa kukatwa na mapanga wakati akitokea katika kituo chake cha kazi usiku.

Aidha, katika taarifa yake iliyotolewa na  Wizara ya Afya, imelaani ukatili huo na kueleza kuwa Serikali kupitia vyombo vyake inafanya ufuatiliaji dhidi ya mauaji hayo na taarifa rasmi itatolewa.

“Wizara ya afya inalaani vikali kitendo hiki cha mauaji ya mwanataaluma ya udaktari na kitendo hiki hakikubaliki kwenye jamii,” imeeleza taarifa.

Siku ya tukio la mauaji ya mtaalamu huyo wa afya inaelezwa kuwa wakati akiwa kwenye usafiri wake wa pikipiki, alikutana na watu waliomsimamisha na kumshambulia kwa mapanga kichwani, mgongoni, mikononi na miguuni.

Send this to a friend