Mauritius yaipiku China kwa uwekezaji Tanzania

0
58

Mauritius imeibuka kuwa chanzo kikuu cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini Tanzania Januari 2024, na kuipiku China, huku takwimu zikionesha mtaji uliongezeka mara tatu katika mwezi huo.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeripoti kuwa mtaji wa uwekezaji kila mwezi, ukiwa ni pamoja na uwekezaji wa kigeni na wa ndani, ulikuwa dola milioni 422.15 [sawa na TZS trilioni 1] mwezi Januari, ikilinganishwa na dola milioni 122.01 [TZS bilioni 310.5] zilizorekodiwa Januari 2023.

Katika kitengo cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDIs), Mauritius imekuwa nchi inayoongoza kwa kuwa chanzo kikuu mwezi Januari baada ya kuleta miradi yenye thamani ya dola milioni 58.78 [TZS bilioni 149.6] ikifuatiwa na China, ambayo wawekezaji waliingiza dola milioni 51.37 [TZS bilioni 130.7].

India inashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo baada ya kutoa miradi yenye thamani ya dola milioni 14.51 [TZS bilioni 36.9].

Send this to a friend