Mawasiliano ya kidijitali yanavyosaidia kutuleta pamoja

0
34

Ugonjwa wa korona (COVID-19) umebadili maisha ya watu wengi kwa namna ambazo hatukutegemea.  Moja ya badiliko kubwa ni lile la kupunguza mikusanyiko, kubaribiana na wengine kuathiri mipango ya safari. 

Bahati nzuri teknolojia ya mawasiliano kama mitandao ya kijamii, video calls na nyingine sawa na hizo zimetusaidia kuendelea kuwasiliana huku tukipunguza mikutano na mikusanyiko. 

Katika wakati huu, kampuni za mawasilino ya simu nchini Tanzania zimefanya kila jitihada kusaidia wateja wake kuendelea kupata huduma bora za mtandao wa intaneti na mawasiliano kwa ujumla. 

Moja ya kampuni hizo ni Tigo Tanzania, moja ya kampuni kubwa za mawasiliano nchini. Huduma ya Tigo Home Internet huwapa wateja wake mtandao wenye kasi na wa kuaminika kuendana na mahitaji yao. Wakati huo huo simu ya Tigo Kitochi 4G yenyewe inawapa wateja waishio kwenye maeneo yenye mtandao wa 4G huduma ya uhakika ya intaneti na kufurahia mitandao kama Facebook, WhatsApp na Barua pepe.

Tigo imesema kuwa inaendelea kufanya kila iwezalo kutoa huduma bora kwa wateja wake. Sasa wateja wa Tigo wanaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja kupitia njia mbalimbali zaidi ya kupiga simu kama WhatsApp, Facebook au Twitter. 

Katika nyakati hizi za changamoto ya kirusi cha korona kuwa na mawasiliano ya kidijitali yenye uhakika ni muhimu pengine kuliko wakati mwingine wowote ule. Ni jambo jema kwamba kampuni za mawasiliano ya simu kama Tigo zinaendelea kuhakikisha hilo linawezekana. 

Send this to a friend