Mawaziri Uganda kuanza masomo ya lazima ya lugha ya Kiswahili

0
33

Baraza la Mawaziri nchini Uganda linatarajia kuanza masomo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kuanzia wiki ijayo ili kuimarisha uwezo wao katika lugha hiyo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rebecca Kadaga wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la pili la mwaka la Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) jijini Kampala.

“Kuanzia Jumatatu, baraza zima la mawaziri litaanza mafunzo ya Kiswahili rasmi. Itakuwa kila Jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi hadi 4 asubuhi kwa mawaziri kuchukua masomo ya Kiswahili,” ameeleza.

Kenya kuzalisha nishati ya nyuklia ifikapo 2038

Ameongeza, “kuhusu suala la lugha ya Kiswahili katika eneo hili, sisi ndio tunafanya vibaya. Hata hivyo katika muda wa takribani mwaka mmoja tutakuwa tukizungumza na kuwaandikia kwa lugha ya Kiswahili.”

Mnamo mwezi Julai, Serikali ya Uganda ilipitisha matumizi lugha ya Kiswahili katika shule za msingi na sekondari baada ya kuifanya kuwa lugha ya pili ya kitaifa.

Send this to a friend