Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameahidi kuwashawishi mawaziri na wabunge kujifunza mchezo wa gofu kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier kufanya hivyo
Amesema hayo jana wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa mabalozi na wataalamu wa nchi mbalimbali ambao ni wachezaji na wanachama wa chama wa gofu nchini kufuatia kumalizika kwa mashindano ya gofu yaliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania yaliyofanyika April mwaka huu Dar es Salaam.
Amesema atawahamasisha wabunge kujifunza mchezo huo ili kuwa timu bora ya bunge ya mchezo wa gofu hali itakayopelekea wabunge hao kuendeleza mchezo huo katika majimbo waliyotoka.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro amewapongeza washiriki hao na kuwaaahidi kuendeleza mchezo huo kwa kuunganisha na utalii wa michezo ili kuhamasisha Mabalozi hao kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
‘” Nawaahidi kuandaa mashindano mengi zaidi ya gofu ambayo nitawashirikisha karibu vivutio vya Utalii ili mkishacheza gofu mnajipumzisha kwa kuwa tembo na simba,” alisema Ndumbaro
Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ametoa wito kwa Watanzania kujifunza mchezo wa gofu huo kwani ni mchezo kama michezo mingine
Amewatoa hofu Watanzania kuwa mchezo huo haubagui ni wa watu wote wenye kipato cha chini na cha juu na sio mchezo wa Watu wa Matajiri na Wasomi pekee