Mayele na Mgunda wang’ara tuzo za Novemba

0
55

Kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kimemchagua mshambualiaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele kuwa mchezaji Bora wa Novemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2022/2023 pamoja na Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda kuwa kocha bora wa mwezi huo.

Mayele amechaguliwa baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Novemba na kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao saba, kati ya hayo matatu ‘hat trick’ akifunga katika mchezo mmoja.

Mchezaji huyo ambaye pia alihusika katika upatikanaji wa bao moja kwenye michezo mitano aliyoichezea Yanga mwezi huo, aliwashinda Moses Phiri wa Klabu ya Simba na Saido Ntibazonkiza wa Geita Gold alioingia nao fainali.

Mbosso aeleza tatizo la moyo linavyoathiri muziki wake

Kwa upande wa kocha Mgunda, amewashinda Hans Pluijm wa Klabu ya Singida Big Stars na Mecky Maxime wa Klabu ya Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali.

Aidha, Kamati hiyo imesema katika mchakato wa kutafuta kocha bora wa mwezi Novemba haikuihusisha Azam FC kutokana na kutokuwa na kocha mkuu katika mwezi huo.

Send this to a friend