Mbagala: Mahabusu wampiga askari na kutoroka

0
55

Zaidi ya mahabusu 20 wametoroka na kukimbilia kusikojulikana kutoka kwenye kituo cha Polisi cha Maturubai mkoani Dar es Salaam walikokuwa wanashikiliwa baada ya kumpiga askari na kuvunja lango la chumba cha mahabusu.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo la Septemba 4 usiku na kusema kuwa wanaendelea kuwatafuta wote waliotoroka ili warejeshwe kuzuizini.

Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Daniel Shila amesema kuwa waliotoroka ni mahabusu wenye makosa madogo madogo waliokamatwa na kwenye doria iliyofanya na jeshi hilo.

Aidha, ameongeza kuwa hakuna silaha iliyoibwa na mahabusu hao baada ya kutoroka.

Send this to a friend