Mbatia awataka Watanzania kuvikataa vyama vinavyofanya siasa za chuki

0
35

Katika kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amewataka Watanzania kuwa makini na vyama vya siasa vinavyofanya siasa zenye kujenga chuki miongoni mwao.

Akiwa mkoani Arusha katika ziara ya kichama, Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo amesema siasa za chuki haina nafasi na kwamba Watanzania wachague viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo.

Aidha, amevitaka vyama vya siasa nchini kutumia hoja kupinga hoja na sio kuendesha siasa ambazo hazifai.

Akizungumzia mutsakali wa siasa za chama hicho amesema kuwa kitaendelea kusimamia siasa za maridhiano katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia lengo la kufikia maendeleo yanayoigusa jamii yote kuanzia ngazi ya chini.

Send this to a friend