Mbeya yafunga mashine za ‘ATM’ za kujipima UKIMWI

0
48

Katika kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI, Mkoa wa Mbeya umefunga mashine maalum ambazo zinaruhusu watu kujipima VVU kwa hiari yao.

Mashine hizi ambazo zimeanza kufungwa katika kumbi mbalimbali za starehe, zinalenga kupunguza maambukizi ya VVU, hasa miongoni mwa vijana.

Mradi huu wa kipekee unatekelezwa na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani PEPFAR na kusimamiwa na shirika la HJFMRI katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Mbeya ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa maambukizi kwa asilimia 14, ikifuatiwa na Iringa asilimia 13 huku Dar es Salaam ikiwa na asilimia 11.

Chanzo: Habari Leo

Send this to a friend