Mbinu 24 za kuwa mtu mwenye ushawishi (influencer) katika mtandao wa Twitter

0
33

Makala hii fupi ihusuyo matumizi ya mtandao wa Twitter kwa wenye lengo la kuwa “influencers” nimeiandaa kwa kupitia majarida mbalimbali ya masoko mtandaoni ambayo washuhuda (reviewers) wengi wanayapa alama za juu kama mwongozo wa wanaofanya uuzaji wa bidhaa au ushawishi kupitia mitandao ya kijamii hasa Twitter. Karibu.

1. Weka picha yako kwenye eneo la profile photo. Mtandao wa Twitter huwa unakupa picha ya yai kwa wale wasiopenda kuweka picha yoyote. Akaunti nyingi Twitter ambazo hubaki kuwa na yai tu huwa haziaminiki na wewe kama unataka kuwa na ushawishi kwa lengo lolote lile lazima uaminiwe kwanza.

2. Andika bio yako kwa kueleweka. Huu ni ule wasifu wako mfupi Twitter unaoandika chini ya jina lako. Tumia maneno ambayo ni mafupi lakini yanakuwakilisha wewe ni nani, unaamini nini, na ikiwezekana usiwe serious sana, weka kautani kidogo lakini ujumbe ubaki. 

3. Pale kwenye header weka kitu ambacho kitavutia. Inaweza kuwa tangazo la biashara yako kama una biashara au hints za kitu unachokipenda. Huo ni kama ubao wako muhimu sana. Utumie. 

4. Chagua username ile @ yako inayoelezea what you are all about. Ni ngumu ila ukiweza hiyo (unless wewe ni celebrity tayari kila mtu anakujua) utakuwa umefanikiwa sehemu kubwa tayari. Kama unauza mayai, handle yako isiwe @nyanya. Unanielewa. Mudi Mabiriani anauza Biriani. Wala huwazi mara mbili.

5. Jitahidi tweets zako ziwe short and clear. Twitter watu hawapendi mambo mengi unless unaeleza stori moja ya kuvutia sana kwenye thread. Science ya Twitter ni uwezo wa kupenyeza ujumbe wako kwenye hadhira yenye muda mchache na mambo mengi.Elewa hiyo sayansi, master it. 

6. Jibu watu, engage na watu wanao-engage na tweets zako. Usijifanye superstar sana. Moderate and good engagement ni jambo zuri na linakupa nafasi kuonekana zaidi na kukua zaidi. 

7. Kuwa na kama orodha yako (list) ya watu ambao hawajivungi sana kwenye ku-engage. Hao ni watu muhimu sana kwenye kuwasha moto na kuipa maisha akaunti yako, tweets zako na nguvu yako Twitter. 

8. Zingatia kanuni za uandishi. Mfano kuanza nafasi baada ya nukta au mkato, kuanza sentensi kwa herufi kubwa na mambo kama hayo. Believe me, hayo mambo madogo ila yanafanya tweets zako kuwa neat na kuvutia. Twitter ni visual game pia so understand and master it.

9. Don’t be too serious. Tweet humor, engage in jokes, amid your business. Take it easy. Relax. 

10. Engage na watu angalao watano kila siku. Kumbuka Twitter ni kutengeneza connections. 

11. Kuna sehemu wakati naongelea kanuni za uandishi nimesema Twitter ni visual game, sasa hapa narudia, Twitter ni visual game na ukiweza changanya tweets zako na picha. Tafiti zinaonyesha tweets zinazoambatana maandishi na picha zina engagement kubwa kuliko zenye maandishi tu au picha tu.  

12. Epuka kurudia rudia tweets za aina fulani. Twitter ni mtandao wa watu wanaokinai vitu haraka. Usiwe unatabirika sana labda sijui uwe celebrity wa namna gani. 

13. Sometimes “live tweet”, uko wapi na unafanya nini na ikiwezekana tupia picha. It’s a game of credibility, unamkumbuka Doto Imeli? I mean be real and be you and share that sometimes, itaku-boost. Ila usizidishe sasa. 

14. Kama una akaunti zaidi ya moja na zote ziko device moja kila wakati kabla ya kutweet hakikisha unatweet akaunti sahihi na ujumbe sahihi. Twitter ukiyakanyaga watu huwa hawasahau.

15. Shiriki kwenye hashtags za jamii kadiri inavyowezekana hasa zile ambazo ni za kujitolea. Msaada wa mgonjwa, msiba, public announcement, etc. It’s called social media, be social.

16. Follow watu kama unataka na wewe waku-follow halafu acha utoto wa kuwa-unfollow baadaye. Credibility is key. Tendea wenzako kama unavyopenda wewe utendewe.

17. Uwe na mpangilio sahihi wa tweets (ratio). Sio 100% ujinga ujinga, au 100% mambo serious, au 100% siasa. Mix that thing up. Kuwa na ratio maana TL yako ina watu tofauti tofauti. 

18. Jifunze lugha ya Twitter na vifupisho. HT, RT, BRB, LOL, LMFAO, etc.  

19. Tumia hashtag kuweza kukusanya kuenea kwa ujumbe wako kirahisi. Mfano kama unauza spea za magari unaweza kutumia #NauzaSpea, inaweza kukufanya ugundua wauza spea wengine wengi zaidi au mtu ambaye amewahi kufanya kitu sawa na hicho na alifeli au kufanikiwa wapi. 

20. Ikibidi PIN your best performing tweet.

21. Usiwe mnafiki. Ukiona kitu sio sema. Twitter/the internet loves real people because it’s full of fake people.

22. Jua mistari ambayo huruhusiwi kuvuka ili usije kutulilia. Mfano usimtukane boss wako eti kesi namba 21 hapo nimesema be real. Find a way to engage them. Be nice. Don’t bully, don’t shit on your own people.  

23. Andaa party sometimes au event, sio kubwa kama ToT Bonanza ila unaweza kufanya na watu wako hata wa Twitter kama watano na kuendelea and all can live tweet. Klout score yake ni kubwa tu hiyo. Idea nakupa. 

24. Kuna applications kibao kama Hootsuite, Falcon, etc unaweza kupanga tweets zako ziruke muda wowote. Wewe unaziandika unaziweka kwenye hizo apps muda ukifika unaotaka zinaruka zenyewe. Inafanya akaunti yako ibaki active twitter hata kama unaendelea na jambo jingine ila pia inakusaidia kuna muda inakuja tweet kali kichwani ila hutaki kuiweka muda huo, ukisubiri unajikuta umeshaisahau. 

Nyingine ngoja nibaki nazo mimi kwa leo. Nifollow Twitter @nyamokomayagilo

**

Mwandishi wa Makala hii amejitambulisha kwa jina la Nyamoko Mayagilo. Anapatikana kwa barua pepe: mayagilo@gmail.com na Twitter kwa kubonyeza lini @nyamokomayagilo

Tunakaribisha makala kwa Swahili Times kwa kutuma kwenda mail@swahilitimes.co.tz


Send this to a friend