Mbinu 5 za kuanzisha mazungumzo na msichana uliyekutana naye mara ya kwanza

0
118

Umekuwa ukitumia njia gani kumshawishi msichana kukubali kuwa karibu na wewe kwa mara ya kwanza?

 

Chochote kitakachotokea kati ya nyinyi wawili kinategemea sana mazungumzo hayo ya kwanza na hisia mtakazoacha kwa kila mmoja.

 

Hizi ni njia 5 za kuanzisha ukaribu na msichana unapokutana nae kwa mara ya kwanza;

 

1. Muda ni muhimu sana

Hili ndilo jambo kubwa zaidi ambalo hutakiwi kuharibu. Inawezekana ukapata matokeo usioyategemea ikiwa unamfuata katika kipindi ambacho hayuko kwenye hali nzuri au akiwa na kundi la marafiki.

 

Njia hii itaamua kukupa usikivu wake au la, na bila shaka inaweza kuongeza au kuathiri mtiririko wako.

 

2. Jiamini

Unapaswa kujiamini bila kiburi, kudharau au kujishusha. Mtazame machoni na wala usitetemeke, kumkaribia mtu kwa mara ya kwanza ni jambo gumu kidogo, lakini ni lazima lifanyike ikiwa unataka kumpata huyo msichana.

 

3. Msifie

Usiache kamwe kumsifia unapozungumza na msichana kwa mara ya kwanza. Kuwa mwangalifu, na kumbuka kusifia kitu kizuri ambacho umekiona kwake muda huo.

Inaweza kuwa macho yake, tabasamu lake, viatu vyake au chochote. Hakikisha tu ni ya kweli na sio ya juu juu.

 

Wanawake wanaweza kuhisi na kutofautisha pongezi za kweli au uongo, pia wanaweza kukosa raha ikiwa unajipendekeza kupita kiasi.

 

4. Maswali ya wazi

Hapa ndipo uwezo wako wa kumshirikisha katika mazungumzo unapoingia. Unataka kumfanya aongee, kwa hiyo muulize maswali yatakayomwezesha kufanya hivyo. Badala ya kusema “una mpango wowote wikendi hii?” (ambayo inaweza kujibiwa kwa kifupi “ndiyo” au “hapana”), sema “Una mpango gani wikendi hii?”

 

Swali linalohitaji jibu lenye maelezo ni bora badala ya lile linaloweza kujibiwa kwa kifupi, ndio au hapana.

 

5. Usikae kupita kiasi

Haijalishi jinsi mazungumzo yanavyovutia, jifunze kuondoka wakati mambo bado yanafurahisha. Usizidishe mazungumzo hadi kumchosha au ukimya usio na maana.

 

Kwa kuondoka kabla mazungumzo hayajaisha, unajipa nafasi kubwa zaidi ya kupata namba yake na kumfanya akukubalie kuwa na wewe.