Mbinu 6 za  kuishi na mwanaume mwenye wivu uliopitiliza

0
86

Zungumza naye
Kuwa na wivu inamaanisha kuna kitu ambacho kinamsumbua, kitu ambacho anahisi utakifanya. Tafuta muda ambao ametulia na umwambie namna ambavyo wivu wake unakukosesha furaha. Mhakikishie kuwa unampenda kisha mshawishi akwambie ni kitu gani hasa ambacho umewahi kukifanya mpaka kumfanya kuwa namna hiyo.

Chunguza
Katika kuongea naye anaweza asiseme ukweli nini sababu ya wivu huo, unachotakiwa kukifanya ni kuchunguza kujua wivu wake unatokana na nini.
Wakati mwingine wivu wake unaweza kuwa hauhusiani na mambo unayoyafanya bali mambo ambayo anayafanya yeye au jinsi alivyo. Chunguza ujue kama shida ipo kwako au kwake, ni muhimu kujua kwanza kabla ya kufanya chochote.

Badilika kama tatizo ni wewe
Inawezekana wewe ndiyo unamfanya awe hivyo, mambo ambayo ulikuwa unafanya kabla au ambayo unayoyafanya sasa, aina ya marafiki unaoongozana nao, jinsi unavyopokea simu, yote haya yanaweza kumfanya kuwa na wasiwasi. Kama tatizo ni wewe basi acha na umuoneshe kuwa umeacha.

Acha kuweka siri na kujitetea kwa vitu vya kawaida
Kama ni ujumbe si lazima ufute kama ni za kawaida, kama ni simu umepigiwa huna haja ya kujificha, kama ni marafiki huna haja ya kukutana nao kwa siri. Kila mara unapofanya vitu kwa siri na unapojaribu kujitetea kwa vitu vya kawaida ndivyo unavyozidi kuondoa imani yake kwako.

Weka Mipaka yako
Mwanaume mwenye wivu atataka ku‘control’ kila kitu katika maisha yako, atataka kukupangia kila kitu. Ni muhimu na ni lazima kuweka mipaka, ni lazima wewe mwenyewe useme kuwa kitu flani siwezi kufanya.

Usikimbilie kuomba msamaha
Endapo unajua hujafanya kosa lolote na umejaribu kuongea naye lakini hakuelewi basi acha kuendekeza kununa kwake na usikimbilie kuomba msamaha kwa jambo ambalo uko sahihi, kwani ukiendekeza kuomba msamaha na kulia kwa kuwa amekukasirikia hatoweza kamwe kubadilika.