Mbinu ya wadukuzi (hackers) katika kudukua akaunti yako Twitter, Instagram au Facebook

0
52
  1. Unapokea barua pepe (e-mail) ya aina hii kwenye anuani yako ya barua pepe hasa kwa wale waliotumia akaunti za barua pepe kujisajili Twitter (wengine hutumia namba za simu). 
  1. Kawaida utapaniki na kutaka kubonyeza hapo palipoandikwa “Unlock my account”. Usifanye hivyo. Kama uko katika browser, kwanza utaona account yako iko sawa, hata ukimuomba rafiki yako akutazamie. Sasa nenda kwenya akaunti yako ya Twitter na logout kwanza. 
  2. Fanya ukaguzi kama e-mail hii ya angalizo kweli imetoka Twitter na si wadukuzi. Unafanyaje? Juu pale palipoandikwa From verify, ukiweka cursor yako juu yake utaona si anuani toka Twitter bali tovuti nyingine kabisa. Tazama chini kushoto kabisa mwa hii picha hapa chini. Utaona barua pepe inayojieleza kuwa ni kutoka Twitter si Twitter.com bali Twttesr.com na barua pepe yenyewe si verify@twitter.com bali verify@twttesr.com
  1. Sababu tayari uli-log out katika browser, uko salama sasa kubofya link hiyo ya palipandikwa Unlock my account. Ukibofya kinatokea hiki hapa chini, kikitaka username yako na password. Hebu kikague. Kwanza anwani unaona juu ni mytweetsnow.com na si twitter.com ambayo ndiyo tovuti rasmi ya Twitter. Ukiendelea na kuweka simu, barua pepe au username yako na password kisha ukabofya log in, mdukuzi aliyetuma link atapata taarifa zako hizo za siri na atachukua akaunti yako na utakuwa umedukuliwa. 

Hii inaweza kukutokea Facebook na Instagram pia. 

Kaa salama mtandaoni!

*Swahili Times Technology Desk*

Send this to a friend