Mbinu zinazotumika kutapeli vijana/wazazi ajira Jeshi la Polisi

0
67

Siku chache baada ya jeshi la polisi kutangaza nafasi za ajira limeripoti kwamba kumeibuka wimbi la matapeli wanaotuma ujumbe na kuwapigia watu simu kuwa wanaouwezo wa kuwasaidia watu kupata ajira hizo.

Jeshi hilo limesema matapeli hao wanadai kwamba wapo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na wengine wapo katika ofisi za makamanda wa polisi wa mikoa na wanaweza kupitisha majina yao ili wapate ajira.

MATANGAZO YA NAFASI ZA KAZI

Matapeli hao akiwemo anayetumia namba 0685643170 wanatafutwa na polisi kwani tayari wameanza kutapeli wazazi na vijana.

Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wananchi na wote wenye sifa za kuomba kutembelea tovuti ya jeshi hilo ili kupata taarifa rasmi, na kwamba waepuke kutafuta njia za mkato. Aidha, wametakiwa kutoa taarifa vituo vya polisi endapo watapata ujumbe au kupigiwa simu na matapeli.

Agosti 18 jeshi hilo lilitangaza nafasi za ajira 3,366 kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) waliopo kwenye makambi hayo.

Send this to a friend