Mbosso aeleza tatizo la moyo linavyoathiri muziki wake

0
60

Mwanamuziki Mbwana Yusuph ‘Mbosso’ amemesema amekuwa akisumbuliwa na shida ya moyo ambayo imekuwa ikimpa maumivu makali pamoja na ganzi kwenye mikono inayosababisha wakati mwingine kumwathiri anapokuwa jukwaani.

Akizungumza na BBC Swahili amesema tatizo hilo ambalo kitaalamu linajulikana kama ‘arteriosclerosis’ alielezwa na wataalam wa afya ambao waligundua mishipa kutoka kwenye moyo inayopeleka damu katika sehemu za mwili imezibwa na mafuta, hivyo kushindwa kufanya kazi vizuri.

“Nikilala usiku naweza nikaamka nikawa nasikia maumivu sana hadi machozi yananitoka, sometimes [wakati mwingine] hadi nalia, nasikia maumivu au napata ganzi za mikono. Mimi mikono yangu muda wote inatetemeka, nikajaribu kuuliza wazazi wangu wakasema ndivyyo ulivyozaliwa hivyo, hata kipindi unakua ulikuwa unavunja vunja vitu, kwa hiyo mara nyingi vitu vingi nilikuwa nafanyiwa,” ameeleza Mbosso.

Ameongeza, “Nakumbuka nilikuwa na tamasha Mbeya nilikuwa natakiwa nitumbuize na gitaa, ulipofika muda nikawa nashindwa kulibeba gitaa kwa sababu mikono ilikuwa inatetemeka sana, kwa sababu nilikuwa na presha ya shoo halafu na yale maradhi yakawa yamenizidia ilikuwa ngumu, nakumbuka ‘manager’ wangu ndiye alikujua kuchukua gitaa akanipa, ndipo nikaweza kushika, nilikuwa nashindwa kuliokota chini.”

Mbosso (27) ambaye kwa sasa nyimbo zake ‘Huyu Hapa’ na ‘Yataniua’ zinafanya vizuri sehemu mbalimbali, ni msanii kutoka lebo ya Wasafi Classic chini ya msanii Diamond akitokea kundi la Yamoto Band.

Send this to a friend