Mbowe adaiwa kutaka kutumia wanajeshi wastaafu kuchukua dola

0
38

Wakili wa utetezi katika kesi ya Ugaidi inayowakabili Freeman Mbowe na wenzake, Peter Kibatala amesema watakuwa na mashahidi wengi akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro na aliyekuwa DC Hai, Lengai Ole Sabaya.

Kibatala amesema hayo mara baada ya kumalizika zoezi la kuwasilishwa kwa maelezo ya mashahidi na vielelezo vya ushahidi vitakavyotumika kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika Mahakama ya Uhujumu Uchumu (Mahakama ya Mafisadi). Upande wa jamhuri umewasilisha taarifa za mashahidi 24.

Jamhuri imesema kuwa katika moja ya vielelezo Mbowe anadaiwa kula njama ya kuwadhuru viongozi wa Serikali akiwemo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya.

Aidha, anadaiwa kuwa alikuwa akitafuta wanajeshi wastaafu, makomandoo na wale waliofukuzwa jeshini ili kumsaidia kuchukua dola.

Send this to a friend