Mbowe ahamishiwa Dar kwa matibabu zaidi

0
40

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewahamishiwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kushambuliwa usiku wa kuamkia leo jijini Dodoma.

Mnadhimu wa Kambia Rasmi ya Upinzani Bungeni, Esther Bulaya amesema baadae wataeleza ni hospitali gani kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai anapelekwa.

Kiongozi huyo alishambuliwa usiku wa kumkia leo wakati akirejea nyumbani kwake majira ya saa sita usiku, na miongoni mwa maeneo aliyoumia ni pamoja na mguu wa kulia.

Viongozi mbalimbali wamefika kumjulia hali Mbowe ambao ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika, Tulia Ackson na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Binilith Mahenge.

Send this to a friend