Mbu wa bara la Asia ahamia barani Afrika

0
60

Wanasayansi wamesema aina ya mbu aitwaye ‘Anopheles Stephensi’ kutoka bara la Asia anayeeneza ugonjwa wa malaria ameenea hadi barani Afrika na kuwa tishio hasa kwa wakazi wa mijini.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha BBC mbu huyo tayari amesababisha visa vya ugonjwa huo kuongezeka nchini Djibouti na Ethiopia, na hivyo kutatiza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Sababu 5 zinazosababisha tatizo la ganzi mwilini

Watafiti wanasema iwapo aina hii ya mbu atasambaa kwa wingi barani Afrika anaweza kuwaweka takribani watu milioni 130 hatarini.

Anopheles Stephensi ni jamii ya mbu ambaye ana uwezo wa kusambaza vimelea vya malaria vya ‘Plasmodium falciparum na P. vivax.’ Mbu hawa huenea zaidi katika mazingira ya mijini.

Send this to a friend