Mbunge Kenya alivyoiibia serikali bilioni 7

0
38

Mbunge nchini Kenya amekutwa na hatia ya kujipatia fedha, $3 milioni (TZS 6.95 bilioni) kwa njia ya ulaghai kutoka kwa wakala wa serikali.

John Wakule amekutwa na hatia katika sakata linalohusu kusitisha tenda ya kununua mahindi kwa ajili ya kuwasaidia waliokumbwa na tatizo la njaa.

Wakule pamoja na mfanyabishara mwenzake Grace Wakhungu wamekutwa na hatia, na sasa wanashikiliwa katika kituo cha polisi jijini Nairobi, wakisubiria hukumu kutolewa Alhamisi, Juni 25.

Endapo atahukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita, atapoteza sifa ya kuwa mbunge.

Kampuni yao ililipwa fedha hizo baada ya kuituhumu Bodi ya Nafaka na Mazao Kenya kwa kuvunja mkataba mwaka 2014. Mahakama imeambiwa kuwa wawili hao waliwasilisha ushahidi wa uongo nyaraka za kughushi.

Send this to a friend