Mbunge: Misafara ya viongozi inakwamisha shughuli za wananchi

0
60

Mbunge Kunti Majala amedai misafara ya viongozi wa juu wa Serikali ambayo hutumia muda mrefu na kuwasubirisha wananchi pamoja na mabasi ya abiria katika maeneo mbalimbali nchini hukwamisha shughuli za wananchi hivyo itafutwe namna bora ya kudhibiti misafara hiyo.

Akizungumza bungeni Dodoma, Kunti ameishauri Wizara ya Mambo ya Ndani kufanya mawasiliano na viongozi wanapotaka kupita eneo husika ili wananchi waendelee na majukumu yao badala ya kutumia masaa mengi kuwasubiri wapite.

Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema misafara hiyo ipo kwa utaratibu maalum ambao pia unasimamia heshima kwa viongozi wa nchi.

ATCL yatangaza mabadiliko ya ratiba kutokana na uchache wa ndege

“Suala la namna ya kudhibiti hilo ni la watendaji ambao wako chini ya mamlaka zinazohusika, kwa hiyo nadhani ingekuwa ni bora tu kwa mheshimiwa mbunge kutoa ushauri tu kwa mamlaka zinazohusika badala ya kuhusianisha na utendaji kazi wa viongozi wetu ambao umewekwa kwa utaratibu unaozingatia heshima ya viongozi wetu hapa nchini,” amesema Mhagama.

Ameongeza kuwa utaratibu huo upo katika ulimwengu mzima ambao umekuwa ukitumika katika kutoa heshima kwa viongozi na kuzingatia utaratibu ambao unatumika katika uendeshaji wa shughuli za viongozi na Serikali ulimwenguni.

Send this to a friend